Tumetumika Sana Asema Gavana Kingi

Gavana wa kaunti ya Kilifi Amason Jefa Kingi ameenddelea kushikilia msimamo wake wakuhakikisha kuwa eneo la Pwani linakua na muungano wa viongozi wa eneo hili ili kuzungumza kwa saunti moja.

Akizungumza katika eneo la Bamba eneo bunge la Ganze Kingi amewataka wakaazi  wa kaunti hio kushirikiana na viongozi ili kufanikisha azimio hilo la kuwa na mwavuli mmoja wa kisiasa.

Gavana Kingi amesema wakaazi wa pwani wamekua wakitumika kwa muda mrefu katika chaguzi zilizopita na sasa ni wakati wa eneo hili kushikamana na kuhakikisha kuwa kunakua na sauti moja ya uongozi na kufanikisha ajenda za maendeleo

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *