Tuko Tayari Kwa Uchaguzi Wa Msambweni Yasema IEBC

Tume ya mipaka na uchaguzi IEBC imesema mikakati imewekwa kuhakikisha kuwa maagizo ya wizara ya afya ya kujikinga na korona yanafuatwa vilivyo kwenye uchaguzi mdogo wa Msambweni.

Akizungumza na wanahabari wakati wa shughuli za kutayarisha vifaa vya kupigia kura msimamizi wa uchaguzi huo mdogo Yusuf Abubakar amesema kuwa vituo vyote vya kupigia kura vimenyunyuziwa dawa kabla ya zoezi la upigaji kura hio kesho.

Abubakar  amesema kuwa wameteua afisa maalum atakaye hakikisha kuwa wapiga kura wanafuata sheria zakujikinga na virusi vya korona wakati wa zoezi hilo la upigaji kura huku akidokeza kuwa tayari kumetengwa sehemu maalum ya kuwashughulikia wale watakaoonyesha dalili za ugonjwa wa covid-19.

Tayari maafisa watakao simamia uchaguzi huo wamepewa mafunzo kabla ya kupokea vifaa vya shughuli hio ya kupiga kura.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *