Tuko tayari kwa michezo yasema timu ya Somali Starlets

Huku shughuli za michezo zikitarajiwa kuanza havi karibuni humu nchini, timu ya Somali Starlets kutoka Mariakani kaunti ya Kilifi imeweka mikakati kabambe ya kuhakikisha wanatimiza masharti yatakayowekwa na wizara ya michezo.
Kulingana na meneja wa timu hio Lilly Rimba Denje nikuwa mikakati iko tayari ya kuanza mazoezi mepesi pindi michezo itakaporuhusiwa kuendelea nchini.
Lilly akiongea na meza na Pwani mwanaspoti amedokeza kuwa japo michezo itakubaliwa kuendelea changamoto yao kubwa ni ukosefu wa ufadhili wa vifaa vya michezo ikiwemo jezi,mipira na kiwanja chakuchezea.
Timu ya soka ya wasichana ya Somali Starlets ilibuniwa mapema mwaka huu na kabla ya janga la korona walikua wameanza vizuri kwa kucheza mechi za kujipima nguvu ambapo waliweza kuitandika Boyani 4-2, wakatoka sare na Miritini 2-2 kabla ya kuichapa Power 3-0.
Kwa sasa wanasubiri tangazo rasmi kutoka wizara ya michezo ili waendelee na mazoezi na kuzidi kuijenga timu hio ambayo iko chini ya ukufunzi wake Said Muta.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *