Trump na Biden Warushiana Cheche za Maneno

Rais Donald Trump wa marekani na mpinzani wake Joe Biden wamebishana vikali kwenye mojawapo wa mijadala mikali zaidi ya kuwania urais katika muda wa miaka mingi. Huku wakibishana na kutusiana wawaniaji hao wawili walizozana kuhusu janga la korona, hali ya wazungu kujihisi bora kuliko watu weusi na uchumi wakati wa mjadala huo uliodumu kwa dakika 90 uliofanyika huko Cleveland, Ohio. Kwa jumla mjadala huo haukuangazia sera wala hatua ambazo wawaniaji hao watachukua wakiwa afisini. Kura za maoni zinaashiria kwamba Biden anaongoza kwa alama moja dhidi ya Trump. Hata hivyo zikiwa zimesalia siku 35 kabla ya siku ya uchaguzi utafiti kwenye majimbo kadhaa muhimu unaashiria kwamba matokeo ya kura baina ya wawaniaji hao yatakaribiana sana.

Rais Trump na mpinzani wake Joe Biden Wanakaribiana sana kwa kura ya maoni kwenye Majimbo ya ushawishi mkubwa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *