Tatizo la maji kutatuliwa Taita Taveta

Kampuni ya kusambaza maji katika kaunti ya Taita Taveta ya Tavevo imeanza kutekeleza mradi wa maji unaogharimu shilingi bilioni 2.5,  uliyofadhiliwa na benki ya dunia kwa ushirikiano na serikali kuu. 

Kaimu mkurugenzi wa kampuni hiyo David Ngumbao anasema mradi huo unalenga kuimarisha huduma za usambazaji maji kaunti hiyo.

Ngumbao amewataka wananchi kuwa na imani na kampuni hiyo kwani inahakikisha kuwa kila mwananchi atafikiwa na huduma za maji.

Kwa upande wake waziri wa maji kaunti hiyo ,Esther Mwanyumba amebainisha kuwa zaidi za nyumba 1000 katika maeneo bunge yote manne zitanufaika na mradi huo wa maji.

Esther aidha amedokeza kuwa mabomba yote ya maji ambayo yaliharibika yatakarabatiwa huku akitoa wito kwa wakaazi kuripoti visa vyovyote vya mabomba ya maji yanayovuja . 0in;margin-bottom:.0001pt;text-align: justify;line-height:14.65pt;background:white

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *