Tanzia:Mbunge wa Juja Francis Munyua aaga dunia.
Mbunge wa Juja Francis Munyua Waititu, maarufu Wakapee, ameaga dunia.
Alikuwa anaugua ugonjwa wa saratani ya ubongo.Familia ilithibitisha kwamba alifariki Jumatatu jioni wakati akipokea matibabu katika Hospitali ya MP Shah jijini Nairobi.
Kutoka kwetu PwaniFM,tunasema Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.