Suluhu ya matatizo ya mmea wa mnazi pwani ni kujengwa kiwanda,asema Owen Baya.

Mbunge wa Kilifi kaskazini Owen Baya amewakosoa viongozi wa kisiasa wa eneo la Pwani waliotangulia kwa kukosa kutetea kilimo cha mti wa mnazi.

Baya amesema ukosefu wa kiwanda cha mnazi cha serikali katika eneo hili kumechangiwa na ubinafsi na tamaa ya viongozi waliokuwa mamlakani tangu jadi.

Amedai kuwa  wakulima wa mmea huo hawajafaidika kwani wamekuwa wakiuza bidhaa zao kwa bei ya rejareja hali ambayo imeathiri pia uchumi wa eneo hilo.

Mbunge huyo sasa ameahidi kutetea mmea huo ili kuhakikisha kiwanda cha mnazi kimejengwa katika eneo la Pwani na kuongeza thamani ya bidhaa zake.

Aidha amedokeza kuwa tayari amewasilisha mswada bungeni kuhusu mmea huo na kuwataka viongozi wengine wa kisiasa kushirikiana naye ili kuhakikisha mswada huo unapitishwa.

Haya yanajiri huku mikakati ya ujenzi wa kiwanda cha pombe ya mnazi  katika eneo la Rabai ikiwa inaendelea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *