Suluhu kwa uhaba wa maji Kilifi

Uhaba wa maji unaoshuhudiwa katika kaunti ya kilifi Mara kwa Mara unasababishwa na uharibifu wa chemichemi za maji katika kaunti hiyo.

Haya ni kulingana na afisa was shirika la KENYA WATER AND SANITIZATION CIVIL SOCIETY (KEWASNET) Vincent Ouma, ambaye amesema harakati za kukata miti na ukulima zinazoendeshwa karibu na chemichemi hizo huchangia uchafuzi na hatimaye kukauka kwa chemichemi hizo.

Ouma ameziomba serikali zote mbili na mashirika kutoa hamasa na mafunzo kwa wakaazi juu ya umuhimu wa kutunza sehemu hizo na atharii zake pindi zitakapokauka hususan wakati huu wa janga la korona ambapo tunahitaji maji zaidi kwa ajili ya kudumisha usafi unaohitajika.

Mtetezi wa haki za kijamii katika shirika la social Justice centre mjini kilifi Erick Mgoja amesema kwamba serikali ya kaunti inafaa kutoa suluhu la kudumu kuhusiana na uhaba wa maji unaoshuhudiwa katika kaunti ya kilifi Mara kwa Mara.

Hata hivyo ameongeza kwamba mbinu za kuvuna na kuhifadhi maji ya mvua husaidia zaidi wananchi wa kaunti hiyo huku akitaka maafisa kwa serikali kutoa mafunzo hayo kwa wakaazi wote wa kilifi.

Serikali ya kaunti ya kilifi imekua ikinyoshewa kidole Cha lawama kwa muda kuhusiana na tatizo sugu la uhaba wa maji unaoshuhudiwa.

Mafuta ya Dieseli yanatarajiwa kugharimu shilingi 94 na senti 63 kwa lita kutoka shilingi 91 na senti 87 ilhali bei ya mafuta taa itaongezeka hadi shilingi 83 na senti 65 kwa likta kutoka shilingi 65 na senti 45.

Picha kwa hisani

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *