Sofapaka kuhamia Wundanyi
Huenda kiwango cha mchezo wa kandanda katika kaunti ya Taita Taveta kikaimarika pakubwa hivi karibuni
endapo klabu ya sofapaka itahamia kaunti hiyo jinsi ilivyoahidi.
Mwenyekiti wa klabu hicho cha sofapaka Ally Kalekwa anasema ameridhishwa mno na mandhari ya uwanja wa Dawson Mwanyumba uliyoko mjini Wundanyi kaunti ya Taita Taveta.
Aidha Kalekwa amedokeza kuwa watahamisha mechi zao za nyumbani kutoka uwanja wa Machakos hadi uwanja huo wa Dawson Mwanyumba huko Wundanyi, pindi shughuli za ujenzi wa uwanja huo zitakapokamilika .
Gavana wa kaunti hiyo Granton Samboja anahoji kuwa kuhamishwa kwa mechi hizo hadi Wundanyi kutaimarisha uchumi katika eneo hilo.
Akizungumza alipoandamana na Kalelkwa na maafisa wengine ili kukagua ujenzi unaoendelea uwanjani humo Samboja anasema Sofapaka itasaidia kuwanoa wachezaj chipukizi katika kaunti hiyo.
Uwanja huo unatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi sita ijayo.