Size 8 amefanya maamuzi ya kumkimbilia Mungu.

Baada ya kutrend wiki nzima kwa madai ya kwamba Dj Mo amekuwa akicheat na ndoa yao kutiliwa shaka size 8 amefanya maamuzi ya kumkimbilia Mungu.
Size 8 amesema kuwa hakuna maana ya kuwa na uchungu au kuonyesha hasira kwani shetani ndio adui Mkuu na hatolaumu mtu yoyote.
Amesema kuwa baada ya mengi kuzungumzwa kuhusu ndoa yake yeye ameamua kufunga na kusali siku tatu.
Ameongeza pia kuwashauri wale wote ambao wanapitia changamoto katika ndoa zao kumgeukia Mungu na kuombea yoyote anayepitia mitihani katika ndoa yake.
Haya yanajiri baada ya mrembo mmoja kuweka wazi kuwa amekua na mahusiano ya siri na DjMo mume wa size 8 kwa miaka kadhaa sasa. Mitandao iliwaka moto baada ya uvumi huo huku mashabiki kila mmoja akitoa lake la moyoni kumuhusu DjMo,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *