Simba marara wa Kenya waanza mazoezi kujiandaa kwa Olimpiki

Timu ya taifa ya raga kwa wachezaji 7 kila upande ya wanawake maarufu kama Kenya Lionesses, imerejea mazoezini kujindaa kwa michezo ya Olimpiki .

Timu hiyo inayofunzwa na kocha Felix Oloo ilipiga mazoezi yake katika uwanja wa RFUEA mjini Nairobi ,baada ya wachezaji wote kufanyiwa vipimo vya Covid 19 .

Kulingana na nahodha wa timu hiyo Philadelphia Olando itawabidi wafanye mazoezi zaidi ili kujiweka katika hali shwari baada ya kuwa nje bila kucheza kwa muda mrefu.

“Kwa sasa itabidi tuongezee bidii mazoezin ili kuimarisha fitness level ili tuwe na uwezo wa kushiriki katika viwango vya kimataifa” akasema Olondo

Upande wake kocha Felix Oloo amesema wasichana hao wanafanya mazoezi kadhaa ikiwemo fitness, strength , conditioning na mental fitness .

Kocha huyo ameongeza kuwa imekuwa vigumu kwa wachezaji wake na kikosi chote kwa Jumla tangu kuzuka kwa janga la Covid mwaka jana na wanatafuta mbinu ya kuiweka timu sawa kutokana na kukosa mashindano ya kuwaweka wachezaji katika hali shwari.

“Imekuwa vigumu tangu kuzuka kwa Covid 19 upande wa kufanya mazoezi lakini tunatafuta mbinu ya kuwaweka wachezaji katika fomu nzuri licha ya kukosekana kwa mashindano.”akasema kocha Oloo

Lioness wamefuzu kwa michezo ya Olimpiki kuanzia Julai mwaka huu baada ya kufuzu makala ya mwaka 2016 .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *