Shule hazitafungwa tena asisitiza Magoha

Waziri wa elimu professa George Magoha,amethibitisha kwamba hakuna mipango ya kufunga shule tena licha ya ongezeko la visa vipya vya maambukizi ya korona.

Waziri aliyasema hayo alipozuru shule mbali mbali katika maeneo ya Mumias na Malaba.

Waziri alisema wanafunzi million 3 wa gredi 4,darasa la nane na kidato cha nne wamerejelea masomo katika awamu ya kwanza ya ufunguzi wa shule.

Akikiri kuwa maambukizi mapya yanaongezeka,waziri alisema wizara ya elimu inashirikiana na ile ya usalama wa kitaifa kufwatilia hali ilivyo.

Kadhalika alipuuzilia mbali madai kwamba wanafunzi katika shule kadhaa wamekosa mjarabu unaoendelea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *