Shughuli ya utowaji Hati miliki

Serikali inatarajiwa kuanza kutoa hati elfu 78 za umiliki wa ardhi kwa wakazi wa eneo la pwani ili kushughulikia swala la maskwota katika eneo hilo.

Katibu mwandamizi katika wizara ya ardhi  Gideon Mung’aro amesema kuwa serikali tayari imeanza kutoa hati elfu  37 za umiliki wa ardhi huko Taita Taveta, hati elfu 13 za umiliki wa ardhi huko  Kwale, hati elfu 21 za umiliki wa ardhi huko kilifi huku Mombasa  na  Lamu zikitarajiwa kupokea hati elfu  3800 na elfu  4000 mtawaliwa. 

Utoaji wa hati hizo za umiliki wa ardhi unatekelezwa chini ya mpango wa kuharakisha utekelezaji wa shughuli. Alisema kuwa serikali pia itaanza kutatua changamoto za ardhi katika kaunti ya Tana ambapo ardhi humilikiwa na jamii. Akiongea huko  Kilifi , Mung’aro pia alitangaza kuwa rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuzuru eneo hilo ili kuzindua shughuli ya utoaji wa hati za umiliki wa ardhi.

Alisema kuwa serikali inalenga pia kushughulikia tatizo la kukosekana kuwepo kwa wamiliki wa nyumba ambalo limekuwa changamoto kubwa kwa wakazi wa eneo la pwani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *