Shimanyula apongeza kurejea kwa Sportpesa

Mwenyekiti wa club ya kakamega homeboyz Cleophas Shimanyula amepongeza kurejea kwa kampuni ya sport pesa nchini kenya huku akiitaka kampuni hio kutoa udhamini kwa vilabu vya kijamii nchini.

Kabla ya kapuni hio kupokonywa leseni ilikuwa inatoa Zaidi ya shilling millioni tano kwa udhamini wa soka nchini.

Siku ya ijumaa sportpesa ilitangaza kurejea tena nchini huku mkurugenzi wake Ronald Karuri akisema kuwa wanapania kuanza mchakato wa kutoa ushirikiano na jamii kwa minajili ya kukuza michezo yote nchini.

Kabla ya sport pesa kuondoka nchini walikuwa wanatoa udhamini wa shilingi milioni 500 kama udhamini wa ligi ya kenya ambapo walidhamini ligi vilabu vya Gor mahia na afc leopards na Nakuru all stars.

Portpesa pia walikuwa na ushirikiano na FKF ambapo walitoa udhamini kwa FKF kwa kuhdamini timu ya Taifa Harambee stars na Dimba la FKF shield cup ambalo mshindi wake aliwakilisha kenya katika dimba la club bora barani Africa.

Kuondoka kwa sportpesa ilikuwa ni pigo kwa vilabu vingi vikiwemo Gor na Afc leopards ambavyo vilishindwa kabisa kuwamudu wachezaji wake wakigeni.

 Vilabu kama vile Sony Sugar Nzoia sugar na Chemilil  vikikosa kushiriki katika baadhi ya mechi walizokuwa wameratibiwa kucheza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *