Serikali Ya Kwale Yahimizwa Kuwagharamia Wagonjwa Wa Saratani

Wanawake wanaougua ugonjwa wa saratani katika kaunti ya Kwale wameitaka serikali ya kaunti hio kuidhinisha mpango wa kugharamia matibabu ya wagonjwa wa saratani.

Wakiongozwa na Abigael Kinywa wanawake hao wamesema wanakabiliwa na hali ngumu kulipa ada za juu za matibabu za ugonjwa huo,ikizingatiwa kwamba bima ya NHIF haisimamii gharama zote za matibabu za maradhi hayo.

Kwa upande wake Phanice Mbwayo mmoja wa waathiriwa hao ameitaka serikali ya Kwale kuzidisha hamasa kwa jamii kuhusiana na  ugonjwa wa saratani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *