Santos FC Kutoka Bamba Yazidi Kutamba

Timu ya Santos kutoka Bamba imefuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya soka ya Bamba kusini.

Timu hio ya Santos kwenye hatua ya makundu iliweza kujizolea alama 10 baada ya kushinda mechi 3 nakutoka sare mecho moja nakuwawezesha kufuzu hatua hio ya robo fainali.

Meneja mkuu wa timu hio Philister Sauti amewapongeza vijana hao akisema kuwa nidham na bidii ndio imechangia kwa ufanisi huo.

Hapo awali wachezaji wa kilabu hii waliahidi kuendelea na mshikano zaidi ili kufanya vizuri katika mashindano haya hali ambayo meneja huyo ameitaja kuwa imefanikisha umbali waliofika katika kipute hicho.

Pia timu ya kina dada ya Santo nayo imeweza kufuzu hatua hio ya robo fainali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *