Naibu wa Rais Dkt William Ruto na Covid 19

Naibu wa rais Dkt. William Ruto amewaomba wakenya kufuata kanuni za serikali zinazolenga kukabiliana na msambao wa virusi vya Corona.

Alikuwa akizungumza katika kanisa la PCEA Thogoto, Kikuyu, katika Kaunti ya Kiambu , katika mazishi ya aliyekuwa katibu mkuu wa kanisa hilo Rev. Peter Kania Kariuki.

Kwa upande wake waziri wa afya Mutahi Kagwe aliyepeleka risala za rambi rambi kwa niaba ya rais Uhuru Kenyatta amesema Rev Kariuki atakumbukwa kwa kusaidia wasiojiweza katika jamii.

Mkuu wa kanisa hilo Rev Julius Mwamba pamoja na katibu mkuu wa NCCK Chris Kinyanjui walisema kuwa wamepoteza nguzo muhimu.Mwendazake ni mmoja kati ya wakenya walioaga kutokana na COVID 19.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *