Rais Uhuru na Raila wawahimiza wakenya kuisoma ripoti ya BBI kwenye ziara yao Kisumu

Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa chama cha ODM, Raila Odinga walizuru katika Kaunti  ya Kisumu, ambako wamewahimiza wakazi kusoma na kuunga mkono ripoti iliyorekebishwa ya jopo la BBI.

Wakati wa ziara hiyo,rais alizindua ujenzi wa uwanja wa michezo wa Jomo Kenyatta katika eneo la Mambo leo unaokisiwa kugharimu  shilling million 415.

Akiongea katika uwanja wa maonyesho wa Kisumu wakati wa hafla ya kuweka jiwe la msingi kwa ujenzi huo,rais alisema ujenzi wa uwanja huo mpya,ni moja ya ahadi alitoa kwa watu wa eneo la Nyanza, ambalo alisema limebarikiwa na kipaji cha mchezo wa soka.

Rais Kenyatta pia alikagua kazi inayoendelea ya ujenzi wa kituo cha kisasa cha biashara katika kaunti ya Kisumu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *