Raila awataka wanasiasa kujiepusha na uchochezi

Kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga ametoa wito kwa viongozi wa kisiasa kutoka mirengo yote kupunguza cheche za kisiasa ambazo amesema zinaweza kuligawanya taifa hili.

Raila badala yake amewataka wanasiasa kueneza jumbe za amani kote nchini.

Akiongea baada ya kukutana na ujumbe wa viongozi kutoka kaunti ya Kajiado katika ofisi yake jijini Nairobi,Raila amesema nchi hii haiko tayari kushuhudia tena umwagikaji damu kama ilivyokuwa baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.

Kiongozi huyo wa ODM alitaja matamshi ya baadhi ya wanasiasa kuwa vichocheo vya ghasia,mtindo anaosema unafaa kukataliwa kwa vyovyote vile na Wakenya wenye nia njema.

Kadhalka Raila amewahakikishia wakenya kuwa mchakato wa kuifanyia marekebisho katiba ungalipo na hivi karibuni kampeni za BBI zinaregelewa kwa lengo la kuwaelimisha wananchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *