PSG wainginza hela nyingi licha ya kukosa kombe la UEFA

Miamba wa soka nchini Ufarasa PSG club  itakayopata pesa nyingi toka kwa michuano ya dimba la club bora barani ulya licha ya kuwa hawajashinda taji hilo musimu huu.

 PSG alipoteza katika fainali ya michuano hio baada ya kupata kichapo cha bao moja kwa bila mikononi mwa Bayern Munich ya Ujerumani.

Kwa mujibu wa jarida la Swiss Ramble PSG watapokea euro millioni 121 nao Bayern Munich watapokea euro millioni 117. Barcelona ni ya tatu na Euro millioni 104, Manchester city itapokea euro milioni 89 na Chelsea watafunga orodha ya tano bora na euro millioni 73.1.

PSG imechukua nafasi ya kwanza kutokana na dili waliosaini na kampuni ya kupeperusha matangazo kwa runinga.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *