Presenters

This image has an empty alt attribute; its file name is GATES-724x1024.jpg
Dalila Athman
Dalila ni mhariri, muandishi wa matangazo ya biashara na mtangazaji wa Uchambuzi na Swala Nyeti kila Jumatatu hadi Ijimaa kuanzia Saa Kumi na Moja asubuhi hadi Saa Tatu Asubuhi.

Ashawahi kufanya kazi na Idhaa ya Deutche Welle (DW) ambapo alijukumika na kuwahoji watu mashuhuri barani Afrika.

Amesomea mawasiliono kutoka chuo cha Technical University of Mombasa (TUK) na ana shahada ya maswala ya maendeleo kutoka Chuo cha Mt. Kenya. Yeye ni wa kwanza katika familia ya wasichana watatu na anapenda kupika.

Facebook:Dalila Athman, Twitter: @AthmanDalila Instagram:dalila
This image has an empty alt attribute; its file name is GATES-724x1024.jpg
Eric Mgenge
Anajulikana kwa jina maarufu kama DJ Gates. Yeye ni MC, na brand ambassador na pia mtangazaji wa Mashav Mashav akiwa na Ken 1GB.

Alikuwa street boy akiwa mdogo lakini hilo halikumzuia kutimiza ndoto yake ya kuwa mtu bora. Gates amesomea uhandisi na Radio and TV production. Ni jamaa ambaye Manchester ikiadhibiwa atavaa dera na mtandio kuja kazini.

Pia ungana naye kwa vibao vya reggae kila siku ya Jumapili 1pm-5pm.

Makinika naye kwenye Facebook: eric Mgenge, Twitter: gatesmgenge IG: Gates Mgenge
This image has an empty alt attribute; its file name is KEN 1GB-724x1024.jpg
Ken 1GB
1GB ni muandishi, mtangazaji wa soka na mtangazaji wa kipindi cha Mashav Mashav. Amesomea mawasiliano katoka chuo cha Technical University of Mombasa.

Na stesheni inapokuwa na tamasha, yeye huwa wakwanza kutambuliwa na wasikilizaji kutokana na kuwa mwepamba mno umbo linaloambatana na jina lake la kisanii la 1GB.

1GB ni wa mwisho katika familia ya watoto wanne. Dada zake wawili wanaishi na babake Zimbabwe na kisha nduguye mdogo anaishi na mamake huko Uganda. Na hadi pumzi zake za mwisho anasema atashabikia Manchester. Nyumbani anashabikia AFC Leopard na Bandari.

Ungana naye kwenye kipindi cha Mashav Mashav kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa sita akiwa na mwenzake Eric Mgenge.

Facebook: Ken Wekesa, Twitter:@Ken1gb Instagram:ken1gb LinkedIn:kentwes