Pesa za NYS zamtumbukia nyongo mkuu wa zamani serikalini

Mahakama kuu imekataa ombi la kutaka kubadilisha uamuzi wa kutaifisha Shilingi milioni 35 kutoka kwa mmoja wa watuhumiwa waliohusika na wizi wa fedha kwenye Huduma ya Taifa ya Vijana (NYS).

Katibu wa zamani wa Mashauri ya nchi za Kigeni James Thuita Mwangi alirudi tena katika Mahakama Kuu akitaka kufutilia mbali uamuzi huo uliotolewa mwezi Aprili mwaka huu, akisema amepata risiti na stakabadhi zinazoonyesha uhalali wa usambazaji wa vifaa aloufanya kwa NYS.

Hata hivyo Jaji Mumbi Ngugi ametupilia mbali maombi hayo akisisitiza kwamba ilikuwa hoja ya kusudi yenye nia ya kuziba mianya katika uamuzi kwani Mwangi alishindwa kupeana stakabadhi hizo mwanzoni mwa kesi hiyo.

Tayari shirika la kutaifisha mali(ARA) kupitia wakala wake,Peter Ngumi limeweka wazi kuwa limekwisha waandikia barua wakurugenzi wa benki za Absa Kenya, Standard Chattered na Equity kuhakikisha wanatuma pesa husika ili ziweze kuhifadhiwa na serikali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *