Nyota Ndogo aeleza sababu ya kuwapenda wanaume wenye umri wa miaka 50 na zaidi

Msaani Nyota Ndogo amesema kuwa anapenda kuwa katika mahusiano na wanaume “wazima”.

Akiwa live kwenye kipindi cha Mashavmashav na Ken1gb Nyota ndogo amefunguka kuwa baada ya kuachana na baba ya mtoto wake wa kwanza alianza kuwa katika mahusiano na wanaume “wazima”.

 Alipoulizwa anamanisha nini akisema wanaume wazima.

“wanaume ninao wazungumzia ni wale ambao wana umri wa miaka 50 na Zaidi mimi nilipoachana na baba ya mtoto wangu nilianza kuwa na mahusiano na mwanaume mzimakwasabbau hao ndio wanaweza kufanya ni jinsi kuwa mwanamke” alisema Nyota.

Vile vile Nyota Ndogo amefunguka kuwa mume wake anawivu sana katika mahusiano yao na anatabia ya kumpigia simu mara kwa mara.

Aidha ameleza kuwa aliamua kumtumia mumu wake katika video yake mpya ya woman kwa sababu ni kitu ambacho mume wake amekuwa akitamani.

“Nakumbuka nikimweleza kuhusu kazi hio alifurahi sana hata siku ya kutayarisha video yeye alikuwa wa kwanza kuamuka na kutaka tuelekee location” alisema Nyota Ndogo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *