Niko tayari kufunga kaunti asema Gavana Mutua

Gavana wa Machakos Dr. Alfred Mutua amesema utawala wake utasitisha huduma zake leo akisema kuwa mfumo wa ugatuzi nchini unatishiwa.

Gavana huyo wa Machakos alisema hatua hiyo inafuatia azimio la baraza la magavana nchini kupitia mwenyekiti wake Wycliffe Oparanya.

Gavana Mutua alisema kwamba ingawaje siyo busara kwa kaunti hizo kusitisha huduma zao,yuko tayari kuwaagiza wafanyikazi wa kaunti yake kutofika kazini kuanzia leo.

Gavana huyo aliongeza kwamba kwa sasa serikali yake haiwezi kulipa mishahara ya wafanyikazi wakiwemo wahudumu wa afya kutokana na uhaba wa fedha.

Alisema janga la Covid-19 liliathiri ukusanyaji wa mapato kwenye kaunti hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *