Nigeria Yaunda Majopo ya Kuchunguza Madai ya Dhuluma za Polisi

Serikali ya Nigeria imeagiza kubuniwa kwa majopo ya majaji katika majimbo yote 36 kuchunguza madai ya dhuluma za polisi. Majopo hayo yatapokea na kuchunguza malalamishi kuhusu dhuluma za polisi, zikiwemo zile zinazohusishwa na kikosi maalum cha kukabiliana na wizi wa kimabavu, al maarufu, Sars kilichovunjwa. Majopo hayo pia yatachunguza visa vya maafisa wa polisi kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya waandaanaji tangu maandaano yalipoanza juma lililopita. Hii ni pamoja na jopo huru la uchunguzi lililobuniwa na tume ya kitaifa ya kutetea haki za binadamu nchini humo. Maelfu ya raia wa nchi hiyo wamekuwa wakiandamana kwenye miji mikuu kulalamikia dhuluma za polisi. Wametoa wito marekebisho ya idara ya polisi na kushtakiwa kwa wale wanaotekeleza  dhuluma hizo.

Polisi Nigeria Washtumiwa Kuwadhulumu raia

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *