Nigeria Yabuni Kifaa cha Kupima Covid 19 Haraka

Nigeria imetengeza kifaa cha  kufanyia vipimo vya Covid-19 ambacho kina uwezo wa kutoa matokeo ya ukaguzi wa sampuli chini ya dakika 40 na ambayo inaweza kutumiwa na hata watu wasiokuwa na ujuzi wa hali ya juu.

Waziri wa afya Olurunimbe Mamora amesema inafanya kazi kwa harakana bei yake ni nafuu mara 10 zaidi ya vifaa vinavyotumika sasa kufanya uchunguzi.

Kulingana na shirika la BBC kifaa hicho bado hakijaidhinishwa na mamlaka inayohusika lakini imetoa matumaini ya nchi hiyo kuongeza juhudi za upimaji.

Mamlaka zinasema kifaa hicho kinachojulikana kama SARS-COV-2 Isothermal Molecular Assay, kilitengenezwa na Taasisi ya Utafiti wa Tiba ya Nigeria.

Nigeria kufikia sasa imewafanyia vipimo vya corona watu 500,000 kati ya watu karibu milioni 200.

Nchi hiyo imethibitisha kuwa na watu 58,000 walioambukizwa virusi vya coronana zaidi ya vifo 1,000. Idadi ya maambukizi ya kila siku imepungua.

Waziri wa afya Olurunimbe Mamora asema Kifaa cha kupima COVID 19 ni Nafuu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *