Nick Mwendwa Apigiwa Debe Kwale

Mwenyekiti wa shirikisho la soka  nchini FKF tawi la kaunti ya Kwale Hamisi Mwakoja amepongeza hatua za kimaendeleo zilizopigwa na uongozi wa sasa wa soka chini ya rais Nick Mwendwa.

Akizungumza mjini Kwale Mwakoja amewaomba wajumbe ambao wanaruhusiwa kupiga kura kuhakikisha wanamchagua Nick Mwendwa tena kama kiongozi wa shirikisho la soka nchini akimtaja kuwa kiongozi ambaye ameleta mabadiliko makubwa kisoka.

Akitaja mifano ya kukua kwa soka la wanawake, kupanda kwa timu ya taifa ya soka harambee stars katika jedwali la soka , soka la vijana pamoja na maswala mengine Mwakoja amempigia upato Nick Mwendwa kwani huku akiwataja wengine kuwa huenda wakairudisha soka ya Kenya nyuma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *