Nick Mwendwa amesisitiza hakuna shirikisho la kaunti ya Mombasa

Rais wa Shirikisho la soka nchini Nick Mwendwa ameendelea kusistiza kuwa kama viongozi wa Shirikisho la soka nchini hawatambui tawi la shirikisho la kaunti ya Mombasa linaloongozwa na Goshi Ali na wenzake akisema kuwa wanaenda kinyume na uongozi wa FKF kwa kujifanyia harakati zao za soka.
Mwendwa akiongea na meza yetu ya michezo amesema wanasubiri mwelekeo wa FIFA ili kuandaa uchaguzi wa viongozi wa soka nchini.
Kiongozi huyo wa FKF amevionya vilabu vinavyojihusisha na uongozi wa kina Goshi akisema hawatatambuliwa kwani FKF haijawahi na haitashirikiana na uongozi huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *