Ni Afueni kwa wakulima wa Lamu

Wakulima wa mazao mbali mbali katika kijiji cha mpeketoni kaunti ya lamu wanakila sababu ya kutabasamu baada ya barabara ya kuingia na kutoka mji huo kufanyiwa ukarabati .

Wafanyibiashara wa mboga na mazao mengine ya shambani wanadai ukarabati huo utafungua uchumi wa eneo hilo pamoja na miji ya Hindi,Witu na mukowe.

Wakulima hao wanadai kuwa ukarabati huo pia utaimarisha usalama wa bidhaa zao wakati wanapozisafirisha. oia, Dennis Chemonges alisema makundi mengi yalijiingiza katika shughuli za kilimo ambazo kwa sasa zimeathiriwa na janga la Covid-19.

Alisema kufikai sasa serikali imetoa shilingi  million 114 kwa makundi mbali mbali yaliyosajiliwa kwenye kaunti hiyo, ili kuanzisha miradi ya kuleta mapato na kuinua hali ya maisha ya watu.

Makundi hayo kulingana na afisa huyo wa maswala ya vijana yamekuwa yakipata kati ya shilingi elfu-50 na elfu- 100 ili kuanzisha biashara ndogo ndogo.

Hata hivyo alikosoa baadhi ya makundi kwa kufurahia janga la Covid-19 ili kuacha kulipa mikopo kama ilivyotarajiwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *