Naibu wa rais William Ruto asema hataacha kusaidia na kwenda kanisani.

Naibu wa rais William Ruto amesema kuwa hatakoma kuunga mkono na kufadhili shughuli za mashirika ya kidini na zile za kuwahamasisha vijana.

Akiwahutubia viongozi wa makanisa kutoka kaunti ya Nyamira waliomtembelea nyumbani kwake huko Sugoi katika kaunti ya Uasin Gishu,  Ruto alisema kuwa hajutii Imani yake.

Wakati huo huo aliwakashifu vikali wakosoaji wake huku akiwapa changamoto ya kujihusisha na shughuli za kuboresha jamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *