Naibu rais awapuuza wakosoaji wake

Naibu rais William Ruto amepulizia mbali madai ya baadhi ya wapinzani wake kwamba ameshindwa kutekeleza majukumu yake kama msaidizi mkuu wa rais.

Akaiongea katika makao yake ya Karen wakati wa hafla ya kuwahamasisha wakina mama,Ruto alisema kuwa hajashindwa kuhudumia taifa hili kama msaidizi wa rais.

Wakati wa mkutano na ujumbe wa wanawake wafanyibiashara kutoka kaunti ya Nairobi, Ruto alisema ametekeleza vilivyo maagizo yote aliyokabidhiwa na rais.

Naibu rais alisema wale wanaosambaza madai hayo wanapaswa kuzingatia majukumu yao ya kuwahudumia wakenya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *