Mwanafunzi Apigwa Risasi Kwenye Mzozo Wa Ardhi Malindi

Kijana mmoja ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi ya Maziwani amepata majeraha mabaya ya risasi katika makabiliano ya polisi yaliyopelekewa na mzozo wa ardhi eneo la Furunzi hapa mjini Malindi kaunti ya Kilifi.

Mbaga Mlewa anadaiwa kupigwa risasi mguuni na maafisa wa polisi na kwa sasa anaendelea kupokea matibabu katika hospitali ya kaunti ndogo ya Malindi.

Walioshuhudia  tukio hilo, wamedai kuwa kuna bwenyenye mmoja amekuwa akiwahangaisha mara kwa mara akidai kuwa mmiliki halali wa ardhi ambayo mamia ya wakaazi wamekuwa wakiishi kwa muda mrefu sasa.

Wakazi hao wamesema bwenyenye huyo anadaiwa kushirikiana na maafisa hao wa polisi kuwahangaisha wenyeji wa eneo hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *