Mwili Wa Mwanafunzi Aliyezama Baharini Waopolewa Lamu

Mwili wa mwanafunzi wa darasa la nane aliyezama cha baharini kwenye eneo la Mpeketoni katika Kaunti ya Lamu Jumapili iliyopita umeopolewa.

Mwili wa Mark Makau mwenye umri wa miaka kumi na minne umeopolewa baada ya kutafutwa na kitengo cha uokoaji kwa siku tatu mfululizo.

Mark alizama na mwenzake mwenye umri wa miaka kumi na tisa ambaye pia ni mwanafunzi wa darasa la nane.

Hata hivyo mwili wa mtahiniwa huyo kwa jina Anthony Kang’ethe uliopolewa siku moja baadaye.

Mili ya wawili hao imelazwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya Kaunti kwenye eneo la Mpeketoni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *