Mwanamume wa Miaka 26 Nigeria Aliyewauwa Wanawake Tisa Ahukumiwa Kunyongwa huku Akikiri kuwaua Wengine

Mwanamume mmoja aliyewaua wanawake tisa kwenye kisa kilichozua hisia kali nchini Nigeria amehukumiwa kifo jijini Port Harcourt. Viongozi wa mashtaka wamesema mwanamume huyo Gracious David-West, mwenye umri wa miaka 26 aliwanyonga wanawake hao kwenye vyumba vya hoteli mbali-mbali nchini Nigeria kati ya mwezi Julai na Septemba mwaka 2019. Jaji Adolphus Enebeli alisema, mwanaume huyo atanyongwa ingawa si kawaida kwa adhabu ya kifo nchini Nigeria kutekelezwa. Adhabu tatu za vifo zilitekelezwa mara ya mwisho mwaka-2016. Mmoja wa wanawake hao alinusurika kunyongwa lakini hakutoa ushahidi kwenye kesi hiyo. Polisi wamesema kuwa mwanamume huyo pia alikiri kuwaua wanawake 15 katika majimbo sita nchini Nigeria. Aidha, mwanamume huyo alidai kuwaua wanawake wengine sita, lakini hakushtakiwa kwa mauaji hayo kutokana na ukosefu wa ushahidi. Baadhi ya wanawake hao walikuwa viruka njia.

Eneo lilotekelezwa uhalifu Nigeria

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *