Mwanamume India Akata Utombo wa Mkewe Kubaini Jinsia ya Mtoto
Mwanamke mmoja mja mzito inchini India amekatwa tumbo na mumewe aliyetaka kufahamu jinsia ya mtoto aliyekuwa tumboni.
Inasemekana alipasua utumbo kwa kutumia kifaa chenye makali cha kukata nyasi.
Familia ya mwanamke huyo inasema jamaa huyo amekuwa akimuhangaisha mkewe akitaka kumuzalia mtoto mvulana. Wawili hao wana mabinti watano na maafisa wa polisi wanasema kutokana na unyama aliotendewa mke huyo alipoteza mtoto wa kiume.
Polisi wamedhibitisha kwamba mama huyo amelazwa katika hospali moja katika mji mkuu wa Delhi na hayuko katika hatari huku mumewe akitiwa nguvuni.
Mila potovu nchini humo zimekuwa zikichochea wanaume kutaka kubarikiwa na mtoto wa kiume.
Hata hivyo bwana huyo amejitetea akidai kuwa ilikuwa bahati mbaya kwa sababu alikuwa akirusha tu silaha hiyo na kisha kwa bahati mbaya kumuumiza mkewe.
