Mwahima Afariki

Aliyekuwa mbunge wa likoni Mwalim Masoud Mwahima ameaga dunia,Mwahima ameaga dunia alfajiri ya leo nyumbani kwake katika mtaa wa vyemani eneo bunge la likoni.

Kulingana na Mwanawe Juma Mwahima , marehemu alifariki baada ya kuugua ugonjwa wa pumu na kufikishwa katika hospitali ya st. Thomas kwa matibabu kabla ya kuaga.

Itakumbukwa kuwa Mwahima alichaguliwa kuwa mbunge wa Likoni mwaka 2007 kupitia chama cha ODM na akahudumu hadi mwaka 2017 ambapo alibanduliwa kaitka kinyang’anyiro hicho na Mbunge wa sasa Bi. Mishi Mboko.

Mwendazake pia aliwahi kuhudumu kama Diwani mwaka wa 1987 hadi 2007 mbali na kuwa Naibu wa Meya katika jiji la Mombasa kuanzia mwaka 1999 hadi 2002.

 Hata hivyo mwahima alikosa kufika mbele ya kamati ya nidhamu ya chama cha odm baada ya kutakiwa kufanya hivyo alipoonekana akishabikia chama cha jubilee.

Mwahima atakumbukwa kwa kutekeleza miradi mbali mbali ikiwemo ujenzi wa barabara za mitaa ambazo hazikuwa zikipitika na kuziweka kabro,kisha ujenzi wa hospitali ya mrima na ile ya bububu,kituo cha zima moto cha shika adabu,shule ya upili ya masoud mwahima katika wadi ya timbwani miongoni mwa miradi mingine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *