Muonekano Wa Shabiggy Wawashtua Mashabiki

Mashabiki wameanza kujiuliza maswali kibao hii ni baada ya msanii aliyetamba na mwanamke si nguo na baba wa kambo Sha biggy kuonekana street akizungusha kahawa akiwa amevalia mavazi yaliochanika.

Baadhi ya mashabiki walionekana wakimpa ushauri msanii huyoa ambaye kwa sasa anatamba na kibao chake kipya cha Jiko wakimwambia ni sawa kuchapa kazi ila anafaa kulinda brand yake kama msanii anayetambulika eneo hili la pwani.

Hata hivyo msanii huyo kwenye comments ameonekana akijibu kuwa kazi hio yakuzungusha kahawa inampatia kipato lakini akaahidi kujiweka vizuri kama walivyomwambia baadhi ya mashabiki wake.

Aidha wengine wanadai kuwa msanii huyo pengine amefulia na anatapatapa kupitia biashara yake hio.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *