Muleee Aruhusiwa Kwenda Nyumbani

Aliyekuwa kocha wa  timu ya Harambee Stars Jacob ‘Ghost’ Mulee ameruhusiwa kwenda Nyumbani kutoka hospitali ya  Aga Khan kufuatia ajali mbaya ya barabarani kwenye barabara ya  Brookside Drive leo asubuhi. Kocha huyo wa zamani ambaye pia anahudumu kwenye kipindi cha radio asubuhi, alisema ameruhusiwa kwenda Nyumbani kwenye mtandao wa twitter. Ghost alikua akielekea kazini asubuhi wakati ajali hiyo ilipotokea. Ajali hiyo ilitokea wakati matatu ilipogonga gari lake alipokuwa akielekea barabara ya Brookside Drive na akakosa kulidhibiti na kugonga chuma iliokuwa karibu. Alipelekwa kwenye hospitali ya  Aga Khan kwa matibabu.

Kocha wa zamani wa Harambe Stars Jacob ‘Ghost’ Mulee

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *