Muigizaji Filmu Chadwick Boseman Aaga Dunia.

Mcheza Sinema wa Marekani Chadwick Boseman, ambaye alijipatia umaarufu kutokana na jina la Black Panther kwenye sinema za Superhero, ameaga dunia.
Familia yake inasema Chadwick Boseman mwenye umri wa maika 43 alifariki kutokana na ugonjwa wa saratani nyumbani kwake huko Los Angeles, akiwa amezungukwa na watu wa familia hiyo.
Boseman hakuwa ametamka lolote hadharani kuhusiana na ugonjwa huo.
Mara ya kwanza, Boseman alijipatia umaarufu kwa kuigiza watu waliobobea katika fani mbali mbali – kama vile mchezaji wa baseball – Jackie Robinson kwenye sinema kwa jina la 42 ya mwaka 2013, na baadaye mwana-Muziki James Brown mwaka 2014.
Hata hivyo, Ni jina la Black Panther katika sinema iliyowasisimua wengi mwaka 2018 ambalo atakumbukwa kwalo.Katika filamu hiyo Boseman anaonyeshwa kama mtawala wa taifa la Wakanda barani Afrika,  – taifa la kubuni ambalo limestawi kuliko mengine yote duniani, katika maswala ya teknolojia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *