Mtoto wa miaka 5 afariki Kwale baada ya kubakwa

Mtoto wa miaka 5 afariki akipokea matibabu katika zahanati ya Mwangulu baada ya kubakwa jana katika Mazingira yasiyoeleweka.

Mwendazake Nyamvula Bora kutoka kijiji cha Tsagulani huko Lungalunga kaunti ya Kwale anadaiwa kufanyiwa unyama huo majira ya saa tano asubui wakati wazazi wake walipokuwa wameenda kwa shughuli zao za kutafutia riziki familia yao.

Akizungumza kwa njia ya simu Balozi Mwabengo ndugu ya baba wa mwendazake anasema kwamba hadi kufikia sasa hawajabaini aliyetekeleza unyama huo na eneo alilobakwa mwendazake kwani alipatikana akiwa mahututi nje ya nyumba yao baada ya wazazi kurejea nyumbani .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *