mshukiwa apigwa risasi Lamu

Polisi huko Lamu wamemuua kwa kumpiga risasi mwanamume anayeshukiwa kuwaficha nyumbani mwake watu wawili walioaminika kuwashambulia maafisa wa polisi katika kijiji cha Siyu juma lililopita.

Kamishna wa kaunti ya Lamu, Irungu Macharia alisema maafisa wa polisi walilazimika kumpiga risasi Bunu Sabaki Shee baada yake kukataa kujisalimisha pamoja na washukiwa hao.

Macharia alisema maafisa wa polisi walikuwa wamekwenda katika kijiji cha Kwasasi kuwakamata washukiwa hao baada ya kupaswa habari na wananchi.

Washukiwa wawili walitoroka wakati Shee akimshambulia mmoja wa maafisa hao wa polisi.

Ijumaa iliyopita, maafisa wa polisi waliokuwa wakitembea kurejea katika kituo cha polisi cha Siyu walijeruhiwa vibaya baada ya kushambuliwa na wanaume watatu.

 Macharia alisema msako dhidi ya washukiwa waliotoroka unaendelea. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *