Mruttu Aliacha Deni Kubwa Asema Gavana Samboja

Malimbikizi ya madeni ya wanakandarasi yaliyowachwa na serikali tangulizi ya kaunti ya Taita Taveta yametajwa Kama sababu ya ukosefu wa maendeleo mhimu yaliyokusudiwa.

Kulingana na Gavana was Kaunti ya Taita Taveta Granton Samboja alirithi madeni ya Jumla ya shilingi bilioni mbili kinyume na ilikuwa imetangazwa na Gavana mtangulizi Kaunti hiyo Mhandisi John Mtuta Mrutu wakati wa hafla ya kupokeza mamalaka ya ugavana.

Samboja amesema deni Hilo limekuwa likizuia utekelezaji wa maendeleo aliyokusudia kuyatekeleza katika uongozi wake, akiungama kuwa tayari amelipa nusu ya deni hilo.

Haya yanajiri huku Baadhi ya wakaazi wa kaunti ya Taita Taveta wakikashifu uongozi wa gavana Samboja kwa kushindwa kufanikisha maendeleo aliyoahidi wakaazi wa kaunti hiyo chini ya uongozi wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *