Mruttu Aisuta Serikali Ya Taita Taveta

Aliyekuwa gavana wa kaunti ya Taita Taveta Mhandisi John Mruttu ameelezea hisia zake kuhusiana na taarifa za kufutwa kazi kwa wahudumu wa afya katika akunti hiyo.

Akiongea mjini Voi Murutu amesikitishwa na swala hilo na kusema kuwa kuwafuta kazi wahudumu hao wa afya sio suluhu la kutatua matatizo yanayoikabili sekta hiyo.

Mruttu ameishauri serikali ya kaunti ya TaitaTaveta kufanya kikao cha mazungumzo na wahudumu hao wa afya ili kuja na mwafaka wa kudumu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *