Mlindalango wa Gor Mahia Levis Opiyo amesitisha kandarasi yake.

Mlindalango wa Gor Mahia Levis Opiyo amesitisha kandarasi yake na timu hiyo ,kutokana na malimbikizi ya mshahara.

Opiyo aliwasili Gor Mahia kutoka Nairobi City Stars mwanzoni mwa msimu mwa mwaka  2020-21 na alitarajiwa kuchukua nafasi ya Peter Odhiambo, aliyeondoka  K’Ogalo kujiunga na  Wazito FC.

Hata hivyo, licha ya kujiunga na timu hiyo Opiyo bado haijaichezea Gor Mahia msimu huu , huku akijumwishwa kwenye kikosi cha wachezaji wa akiba kwenye mchuano wa ligi ya mabingwa Barani Afrika dhidi ya APR  ya Rwanda, baada ya mlindalango Boniface Oluoch kuugua.

Opiyo tayari ameiandikia  Gor Mahia barua huku akitaka kuruhusiwa kuondoka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *