Minzani ya haki

Mwalimu mmoja wa shule ya chekechea nchini China amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani kwa kosa la kusababisha kifo cha mtoto mmoja baada ya kuwapa zaidi ya watoto 25 uji uliokuwa na sumu.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya taifa hilo Wang Yun alikamatwa na polisi mwaka jana baada ya kuwapa watoto 25 wa shule moja ya chekechea mjini Jiaozuo,uji  uliokuwa na sumu.

Mahakama iliomhukumu Wang ilisema kuwa  alitia sumu aina ya sodium nitrite kwenye uji wa watoto wa shule ya chekechea ya rafiki yake ili kulipiza kisasi tofauti kati yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *