Mikakati Yakuundwa Kwa Chama Pwani Imeshika Kasi

Mikakati imewekwa na Muungano wa wazee wa kaya ili kushinikiza kuundwa kwa chama kimoja Cha kisiasa kitakachotambulika kitaifa na kuwakilisha wapwani katika siasa za nchi.

Kulingana na Tsuma Nzai ambaye ni mshirikishi wa muungano huo, tayari hatua za mwanzo zimefanikiwa ikiwemo kuundwa kwa baraza la wazee litakalo wakilisha kaunti zote 6 za ukanda wa pwani.

Hata hivyo mmoja wa wazee hao Erastus Kubo amesema kuwa baraza hilo litaweza kushirikisha viongozi mbalimbali wa kisiasa hapa pwani ili kupata maoni na sera zao ili waweze kupata mwelekeo mwafaka wa uchaguzi ujao wa mwaka 2022.

Hisia mseto zimekuwa zikizuka miongoni mwa viongozi wa kisiasa eneo la pwani huku baadhi ya viongozi wakiwa tayari wamejitoa peupe kutokubali  kuunga mkono mchakato huo huku wakisema litazua uhasama miongoni wa wakaazi wa eneo la pwani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *