Mikakati ya maambukizi ya Covid-19 Uholanzi

Wakazi wengi nchini Uholanzi,kwa mara ya kwanza watashauriwa kuvaa barakoa wanapotoka nje,taifa hilo linaporatibu sheria madhubuti za kudhibiti wimbi la pili la msambao wa ugonjwa wa Covid-19.

Ikilinganishwa na nchi jirani,Uholanzi haijatangaza hatua madhubuti za kukabiliana na virusi vya korona kufikia sasa.

Kwenye hotuba iliotolewa kupitia runinga ya kitaifa,waziri mku wa nchi hiyo  Mark Rutte alielezea hali ilivyo katika miji mitatu mikubwa nchini humo ya Amsterdam,Rotterdam na The Hague,huku akisema hatua za haraka zinapaswa kuchukuliwa kudhibiti msambao wa ugonjwa wa Covid-19.

Takriban watu 3,000 wanaambukizwa virusi hivyo kila siku katika taifa hilo lenye idadi ha watu milioni 17.

Hatua hizo mpya zitaanza kutekelezwa leo na zitadumu kwa muda wa wiki tatu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *