Mgombea wa Urais Zanzibar Azuiliwa Kufanya Kampeni

Tume ya uchaguzi huko Zanzibar imemzuia mwaniaji mmoja wa urais wa upande wa upinzani kufanya kampeni katika muda wa siku tano zijazo.

Maalim Seif Sharif Hamad wa chama cha ACT Wazalendo amekuwa mwaniaji wa pili wa upinzani nchini humo kuzuiwa kufanya kampeni na tume hiyo.

Alishtumiwa na chama pinzani cha Demokrasia Makini, kwa kukiuka kanuni za uchaguzi.

Anaweza kuwasilisha rufaa kupinga hatua hiyo.

Chama chake kilisema kitaandaa mkutano leo kujadili swala hilo kabla ya kutangaza msimamo wao.

Mwanzo wa mwezi huu , Tundu Lissu,ambaye ni mwaniaji wa urais wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Chadema,alizuiwa kufanya kampeni kwa kipindi cha siku saba.

Maalim Seif Sharif Hamad wa chama cha ACT Wazalendo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *