Mchungaji Mbakaji Ahukumiwa Kifungo Cha Miaka 140 Jela
Mchungaji katika eneo bunge la Ndia, Kaunti ya Kirinyaga ambaye alikiri kosa la kuwabaka na kuwapa ujauzito watoto wake wa kike wa umri wa miaka 14 na 16 amehukumiwa kifungo cha miaka 140 jela.
Huklumu hii imetolewa na hakimu mwndamizi wa Baricho Anthony Mwicigi, ambapo jamaa huyo alipewa kifungo cha miaka 70 jela kwa kwmbaka kila msichana.
Mahakama iliamua kwamba adhabu hiyo itaendelea mfululizo, .
Mshtakiwa huyo mwenye umri wa miaka 51 alikiri kosa hilo Januari 5 na alirudishwa rumande hadi Alhamisi, Januari 7.
Alimlaumu shetani kwa makosa yake na akaomba msamaha watoto wake .
Hakimu Mkuu Mwandamizi Anthony Mwicigi alisema mchungaji huyo alikuwa amehukumiwa kwa kukubali kwake mwenyewe hatia na akaamuru kwamba hukumu dhidi ya mchungaji huyo ifanyike leo.