Mbunge Michael Kingi awaonya Wanakandarasi kwa Kuwabagua Wenyeji Kiajira.

Mbunge wa Magarini kaunti ya kilifi Michael Kingi amewataka wanakandarasi waliokabidhiwa jukumu la kuendeleza miradi ya ujenzi katika eneo hilo kutowaajiri watu wa vibarua ambao sio wakaazi wa maeneo yanayo endelea kujengwa.

Akizungumza katika eneo bunge hilo baada ya kuzindua miradi ya ujenzi wa madarasa katika shule 8 Kingi ametaja hatua hiyo Kama itakayo wasaidia wanajamii hao kukimu mahitaji yao hasa wakati huu wa janga la korona.

Hata hivyio, mbunge huyo ameelezea kuwa wapo baadhi ya wakaazi wa maeneo  hayo ambao wako na ujuzi wa kufanya baadhi ya kazi katika ujenzi huo.

Hata hivyo kwa upande wake mwenyewe kiti wa hazina ya CDF eneo la Magarini Samson Kombe amehoji kuwa miradi hiyo itagharimu kima Cha zaidi ya shilingi milioni thelathini na kuongeza wangali wanasubiri idhini ya kuendelea na ujenzi wa maabara katika baadhi ya shule za upili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *